Saturday, 13 May 2017

Mambo 5 yatakayokufanya kuanza kula tunda la topetope

Tope tope ni moja ya tunda ambalo si rahisi sana kulikuta kwenye majokofu ya watu au kwenye orodha ya matunda mara baada ya kula.

Pamoja na kwamba tope tope linaladha nzuri na linafaida zake ndani ya mwili, lakini wengi hawalitumii sana hivyo leo nimeona nikupatie hizi faida zake kadhaa huenda zitakufanya uanze kulitumia tunda hili

Miongoni mwa faida za tunda hili ni pamoja na hizi zifuatazo:-


Tope tope limesheheni vitamin C imbayo husaidia kuimarisha kinga za mwili na hivyo kumfanya mtumiaji kuepuka kusongwa na magonjwa mara kwa mara.

Pia tope tope lina kiasi cha vitami A ambayo hulifanya tunda hilo kuingia kwenye orodha ya matunda yenye uwezo wa kuboresha na kulinda afya ya ngozi na nywele.

Aidha, tope tope pia limesheheni madini ya 'potassium', ambayo nayo husaidia miili yetu kuondokana na tatizo la maumivu ya hapa na pale ya mifupa.

Kwa wale wenye shida ya maumivu ya mifupa hasa sehemu za maungio 'joint' wanapotumia tunda hili mara kwa mara huweza kuwa msaada kwao katika kuondokana na tatizo hilo kutokana na kuwa na madini ya 'magnesium' ndani yake.

Tunda hili pia lina nyuzinyuzi 'fiber' za kutosha na hivyo kusaidia kurekebisha mfumo wa mmeng'enyo wa chakula tumboni na kuepuka tatizo la ukosefu wa choo.


Kwa maelezo zaidi au ufafanuzi kuhusu namna ya kulitumia tunda hili kwa manufaa ya kiafya unaweza kutupigia kwa simu namba: 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment