Sunday, 7 May 2017

Mambo 6 ya muhimu unayopaswa kufanya kwenye weekend yako

Inapofika siku za wikiendi yaani Jumamosi na Jumapili watu wengi hupata nafasi ya kupumzika na kufanya mambo yao binafsi.

Wapo ambao hutumia siku za weekend kwa kutulia nyumbani tu, huku wakijiandaa na kujipanga vyema ili kuanza wiki ijayo vizuri.

Siku kama ya leo Jumamosi itapendeza kama ukiitumi kwa kukamirisha kazi zako muhimu hasa zile za nyumbani.

1. Tumia weekend yako kufanya usafi kwa ujumla, inawezekekana ikawa ni usafi wa kufua nguo, kusafisha nyumba, vyombo pamoja na kufagia, ni vyema ukajitahidi siku za weekend ukawa unafanya usafi wa kutosha na wakuridhisha kabisa kwasababu mara nyingi katikati ya wiki huwa ni ngumu kupata muda wa kuyafanya hayo tena.

2. Tumia weekend yako pia kukamirisha zile kazi zako ambazo ulishindwa kuzikamirisha katikati ya wiki.

3. Ikiwa mambo yako yote muhimu na ya lazima uliyakamirisha katikati ya wiki na yote yapo sawa, basi weekend yako itumie kwa kufanya mambo mapya unayopendelea kufanya au kujifunza. Mfano kupika, kuogelea n.k

4. Kama wewe ni mwanafunzi, ni vyema ukatumia wikiendi yako kumalizia kazi za shuleni kama ni homework au assignments.

6. Ukiwa na nafasi pia unaweza kuwakumbuka watu wako wa karibu kama ndugu, jamaa na marafiki kwa kuwatembelea au kuwasiliana nao. Weekend hii kama una nafasi waonyeshe ndugu, jamaa na marafi kuwa unawajali na kuwapenda kwa kuwatembelea au hata kuwatumia salamu kwa njia ya SMS na kuwapigia simu.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment