Tuesday, 23 May 2017

Mambo manne yamsingi kuhusu maji ya nazi

Si rahisi kwa kila mtu kufahamu kuwa maji ya nazi huwa na faida zozote ndani ya miili yetu na ndio maana hata wakinamama huyamwaga tu maji hayo mara wanapopasua nazi.

Nadhani wengi wetu tunafahamu kuwa kinamama wanapokuwa na ujauzito huwa ni wakati ambao mama huhitaji kupata vyakula tofauti tofauti kwa ajili ya ukuaji wa mtoto aliyeko tumboni.

Licha ya uhitaji wa vyakula hivyo, lakini pia wakati wa kipindi hicho pia kinamama wajawazito kuna baadhi ya vyakula hujikuta wakishindwa kuvitumia kutokana na sababu mbalimbali.

Leo nahitaji tuelezane kuhusu faida za maji ya nazi kwa kinamama wajawazito:-

1. Husaidia kuimarisha kinga za mwili
Maji ya nazi huwa na viongeza kinga mwili vya asili ndani yake 'natural immunity booster' pia unywaji wa maji hayo huenda kusaidia kuimarisha kinga za mwili za mtoto tumboni na kumsaidia kupambana dhidi ya maambukizi mbalimbali.

2. Husaidia kuboresha mmeng'enyo wa chakula
Mara nyingi kina mama wajawazito hukubwa na tatizo la kukosa choo, hivyo wanapoamua kutumia maji ya nazi huweza kusaidia kuondoa tatizo hilo pia.


3. Hupunguza madhara ya kiungulia
Baadhi ya kinamama wakati wa ujauzito pia husumbuliwa na hali ya kiungulia mara kwa mara hali ambayo inaweza kupunguzwa na maji ya nazi pia.


4. Huimarisha ufanyaji kazi wa figo mwilini
Hii ni kutokana na maji haya ya nazi kuwa na madini ya potassium na magnesium ambayo huenda kuisaidia figo kufanya kazi zake vizuri ndani ya mwili.

Zingatia
Mama anaweza kutumia maji haya ya nazi angalau glasi mbili kwa siku yaani asubuhi na jioni

Kumbuka kuwa pia tunaweza kukushauri kuhusu matumizi ya lishe bora na vitu vya asili tupigie sasa kwa simu namba +255 716 300 200/ +255 769 400 800/ +255 784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment