Friday, 12 May 2017

Mambo matano utakayoyapata kwa kula kiafya

Featured Image
Wataalam wa afya na lishe wamekuwa wakieleza mara kadhaa umuhimu wa kula kwa kuzingatia mlo bora na wenye virutubisho muhimu.

Tunapozungumzia kula kiafya inamaana ni kula vyaula vyenye uwezo wa kuupatia mwili wako mahitaji yake yote muhimu na kuwa na uimara zaidi.

Ninazo hapa faida kadhaa za kula kiafya karibu tuzifahamu kwa pamoja msomaji wangu kupitia mtandao wako pekee huu wa habari za kiafya wa www.dkmandai.com unaosimamiwa na kampuni ya Mandai Products Company ltd.

1. Unapokula kiafya tambua kuwa unajihakikishia ubora wa afya yako ya moyo.
, kwakuwa mtu anayekula kiafya huzingatia mafuta bora ya kupikia na kutokula vyakula vyenye mafuta mengi na vilivyoungwa kwa chumvi ngingi hasa ya mezani.

2. Mtu anayekula kiafya muda wote huwa na afya bora ya mifupa pamoja na meno.

3. Mtu anayekula kiafya huwa na afya bora ya akili. Hii ni kwasababu virutubisho bora husaidia kuimarisha mzunguko wa damu kwenye ubongo.

4.Ulaji mzuri husaidia kuwa na uwito wa mwili unaotakiwa kiafya

5. Kuwa na maisha marefu zaidi ambayo hayana msongo wa magonjwa ya hapa na pale.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment