Thursday, 4 May 2017

Mbinu 2 za kutumia kidogo ulichonacho kufika kwenye kilele cha mafanikio


Kufikia malengo yako unahitaji uwe na uwezo wa kutumia ulichonacho kwa sasa ili uweze kuzalisha kile ambacho unakitafuta.

Kama wewe ni mtu ambaye umeajiriwa kwa sasa na una malengo ya kujiajiri inamaanisha unatakiwa kutumia pesa unazolipwa kwa sasa,maarifa unayoopata kwa sasa na “connection” ambazo unazipata kwa sasa ili uweze kufika kule unakotaka.

Kama wewe una biashara ndogo kwa sasa na unataka kuikuza biashara yako iwe kubwa sana kuliko ilivyo sasa,unatakiwa kutumia faida unayopata kwa sasa ili iweze kukusaidia kutengeneza mtaji mkubwa wa baadaye.

Naomba leo utambue kuwa watu waliofanikiwa ni wale ambao waliamua kutumia kidogo walichonacho kwa sasa ili kiweze kuwazalishia na kufikia kikubwa ambacho wanakitafuta.

Zifuatazo ni njia za kupita ili uweze kutumia kidogo chako cha sasa kuzalisha kikubwa unachokitafuta:

1. Acha kudharau kidogo ulichonacho
.

Kosa kubwa ambalo watu wengi huwa wanalifanya katika maisha yao ni kudharau kazi au biashara ya wakati alionao sasa na kuifanya ilimradi tu. Hii inamaanisha kuwa,watu wengi kwa kila wanachofanya kwa sasa wanafanya kama vile hakina maana kabisa na ukiwauliza wanasema wanasubiria kitu kikubwa zaidi/Kazi nzuri zaidi.Matokeo yake ni huwa ni ngumu kwao kufanikiwa kumbuka kama kidogo umeshindwa kukilinda basi kikubwa huwezi kabisa.

Kumbuka kuwa ni makosa makubwa sana kudharau kazi yako ya sasa au biashara unayoifanya hata kama ni mbaya au haikidhi

2. Jiwekee akiba


Hakikisha unajiwekea akiba ya baadaye.Kati ya tatizo kubwa ambalo watu wengi linawakabili ni kushindwa kutunza akiba kwa kipato chao cha sasa kwa kisingizio kuwa wanachopata ni kiwango kidogo sana. Jambo unalotakiwa kujua ni kuwa na nidhamu ya fedha inajengwa kwa uwezo wako wa kutumia vizuri kidogo ulichonacho.

Kwa ushauri zaidi wasiliana nasi kwa simu namba +255 716 300 200, +255 769 400 800, +255 784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment