Thursday, 25 May 2017

Mvua zimekata, inawezekana zimekuachia fangasi za miguu tumia njia hii asili kuzimaliza

Najua kwamba maeneo mengi ya nchi mvua zimenyesha sana hivi karibuni sasa sehemu nyingi zimepungua kwa kiasi kikubwa.

Lakini kutokana na hali hiyo ya mvua wengi watakuwa wamejikuta wakikumbwa na matatizo ya fangasi hasa za miguuni, hivyo basi leo nimeona nikwambie kuhusu hii njia asili mojawapo ya kumaliza tatizo hilo.

Moja ya njia hiyo ni matumizi ya kitunguu swaumu, ambacho unatakiwa kufanya ni kusaga kitunguu swaumu kisha utapaka sehemu iliyoathirika yaani kwenye fangasi.

Fanya zoezi hilo kwa siku 3 hadi 4 na utaona mabadiliko lakini kama unaweza kupata mafuta yake ya kitunguu swaumu itakuwa njema pia.

Kwa ushauri zaidi tupigie kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

2 comments:

  1. doctor nauliza kuhusu fangasi za sehemu za sili na matibabu ya UTI

    ReplyDelete
    Replies
    1. Asante kwa kutembelea tovuti yetu kuhusu hilo swali lako unaweza kuongea na mimi moja kwa moja kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300 na nitakueleza vizuri kuhusu fangasi za sehemu za siri na U.T.I kwa ujumla wake

      Delete