Wednesday, 24 May 2017

Mwanamke: fahamu athari hizi za pombe ambazo zitakufanya usinywe tena


Utafiti mpya unaonyesha kuwapo kwa uhusiano kati ya unywaji wa pombe miongoni mwa wanawake na ongezeko la kupata na saratani ya matiti.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka na mfuko wa utafiti wa saratani ni kuwa nusu glasi ya mvinyo au bia kwa siku huongeza uwezekano wa kupata saratani ya matiti.

Mbali na hayo, utafiti huo pia unaonesha kuwa mazoezi ya mara kwa mara huweza kusaidia kupunguza hatari ya kupata maradhi hayo ya saratani.

Inaelezwa kuwa saratani ya matiti ndiyo huwakumba zaidi wanawake nchini Uingereza huku mmoja kati ya wanawake wanane wakipatwa na ugonjwa huo katika maisha yao

Chanzo: BBC Swahili

No comments:

Post a Comment