Wednesday, 24 May 2017

Nimekusogezea hii njia asili kwa wewe mwenye U.T.I

Ugonjwa wa UTI kitaalamu huitwa “Urinary Tract Infection” ni ugonjwa ambao huathiri mfumo wa kutengeneza na kutoa mkojo nje ya mwili. 

Maambukizi ya mfumo huu wa mkojo yasipopata tiba haraka huweza kuwa na madhara makubwa zaidi na hata kusababisha kusambaa hadi kwenye figo zako.

Leo naomba kueleza kuhusu hii njia asili ya kutumia chai ya tangawizi kupunguza madhara ya tatizo hili la U.T.I

Unachotakiwa kufanya ni kupata tangawizi kisha isage halafu changanya na maji kiasi cha kikombe kimoja kisha iweke jikoni hadi ichemke kabisa.

Baada ya hapo tumia chujio kuchuja mabaki ya tangawizi kisha kunywa yale maji yake kama chai hivi. Njia hii itakusaidia kukupa ahueni kwa wewe mwenye tatizo hili la U.T.I

Pamoja na hayo, kumbuka kuwa matumizi ya tangawizi husaidia pia kuimarisha kinga zako za mwili na hivyo kukuweka mbali dhidiya magonjwa mengine.

Zingatia
Uaweza kufika hospitali iliyokaribu nawe kwa msaada zaidi mara unapoona tatizo bado linaendelea au tupigie simu kwa namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 kwa ushauri zaidi.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment