Wednesday, 24 May 2017

Nimekuwekea hapa faida zote za papai ikiwemo na ile ya kupunguza uzito


PAPAI ni tunda lisilo geni miongoni mwa Watanzania walio wengi. Ardhi yenye rutuba inaifanya Tanzania kustawisha aina nyingi ya matunda likiwemo papai.

Asili ya papai ni Kusini mwa Mexico na Amerika ya Kati. Hata hivyo, kwa sasa tunda hilo linapatikana sehemu mbalimbali duniani.

Baadhi ya watu wamekuwa wakilitumia papai kutatua tatizo la kukosa au kulainisha choo. Hii ni kwa sababu nyuzinyuzi yaani 'fiber' ambazo zinapatikana katika papai husaidia umeng'enyaji wa chakula tumboni.

Papai pia linapotumika vizuri linasaidia watu wenye uzito mkubwa kuondokana na hali hiyo. Uwezo huo unatokana na tunda hilo kuwa na kirutubisho kiitwacho 'calories' na 'fiber'.

Mbali na faida hizo, pia papai husaidai kuimarisha kinga za mwili na kumfanya mtumiaji kutosongwa na magonjwa mara kwa mara.

Inaelezwa kuwa papai moja lina asilimia 200 ya mahitaji ya kila siku ya vitamin C, hivyo kuufanya mwili kujenga kinga imara zaidi.

Kwa watu wenye matatizo ya kisukari wanashauriwa kutumia papai kwani ni miongoni mwa matunda yenye kiwango cha sukari cha chini, licha ya kuwa ni tamu kwa ladha.

Ulaji wa papai pia husaidia kuimarisha uoni, hii ni kutokana na kuwa na vitamin A ya kutosha.

Ni wazi kuwa hakuna mtu anayetamani kupoteza uwezo wa kuona kutokana na sababu ya aina yoyote iwe ni umri au kuzorota kwa uwezo wa seli, hivyo unaweza kutumia papai ili kuepuka matatizo ya macho ikiwemo uoni hafifu.

Aidha, papai ni moja ya matunda yanayosaidia kuboresha afya ya ngozi kwa kuiacha ikiwa katika hali nzuri hususan katika kuondoa mikunjo katika ngozi.

Ili tunda hili likusaidie kutunza ngozi yako, unachopaswa kufanya ni kuchukua kipande kimoja cha papai, kisha changanya na unga wa ngano kijiko kimoja halafu tumia mchanganyiko huo kwa kuupaka sehemu iliyoathirika (yenye mikunjo).

Kisha uache mchanganyiko huo mwilini mwako kwa muda wa dakika zisizopungua kumi halafu nawa vizuri kwa maji safi na salama.

Fanya hivyo angalau mara moja kwa siku ikiwezekana usiku kabla ya kulala, na baada ya siku kadhaa utaanza kuona mabadiliko katiko ngozi yako.

Mbali na faida za tunda hilo, pia mizizi ya mpapai (mmea wa papai) inapochemshwa ina uwezo wa kutoa ahueni kwa mgonjwa mwenye shida ya mawe kwenye figo.

Mgonjwa huyo anapaswa kuchemsha mizizi hiyo kisha kusubiri ipoe halafu anywe nusu kikombe asubuhi na jioni kila siku, lakini pia mizizi hiyo ina sifa ya kutuliza maumivu ya kibofu cha mkojo, ambapo mhusika atatakiwa kunywa mchemsho wa mizizi hiyo.

Pia mizizi ya papai inaelezwa kuwa ni msaada mkubwa wa kuondoa maambukizi katika njia ya mkojo. Katika hilo mhusika atakunywa mizizi kama ilivyoainishwa hapo awali.

Kama hiyo haitoshi, pia mbegu zake pia zinaposagwa na kukaushwa katika kivuli na kisha kuwa katika hali ya unga laini ukitumiwa husaidia kuondoa tatizo la minyoo, ugonjwa unaowapata watu asiozingatia usafi.

Kwa ushauri zaidi tupigie kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment