Tuesday, 2 May 2017

Njia 2 rahisi za asili za kutibu jeraha kwa haraka

Habari za leo mdau wa www.dkmandai.com bila shaka umzima wa afya tele leo, lakini kama utakuwa haupo vizuri labda unaumwa basi tovuti hii pia inaweza kukusaidia kukupa njia za kumaliza tatizo lako kupitia ushauri wetu pia. Karibu sana

Moja ya mambo ambayo napenda kuzungumzia kwa sasa ni kukufahamisha mambo ya kufanya pale unapopatwa na jeraha au kidonda.

Kwanza kabisa ni vyema kutambua kwamba kila unapopatwa na jeraha fahamu kuwa unakuwa upo katika hatari ya kupatwa na maambukizi mengine kupitia jeraha hilo, hivyo ni vyema ukazingatia kutibu jeraha mapema kabla halijawa chanzo cha matatizo mengine kwako kiafya.

Huenda labda ukawa nyumbani unafanya shughuli zako na bahati mbaya ukajikata na kisu na kusababisha jeraha au chochote kile kikakufanya kupatwa na jeraha basi usipate shida fanya haya yafuatayo:

1. Asali
Asali ni moja ya suluhisho nzuri pale unapopatwa na jeraha unachopaswa kufanya paka kiasi cha asali kwenye jeraha hii itasaidia kukuepusha kupatwa hata na maambukizi mengine kupitia jeraha lako.

2. Ukwaju.
Ukwaju ni njia nyingine ya kukabiliana na majeraha madogo madogo (vidonda) na huu ukwaju huweza kusaidia kuzuia utokaji wa damu zaidi kwenye jeraha.

Kwa maelezo zaidi usisite kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0769 400 800/ 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment