Friday, 5 May 2017

Njia 4 za asili za kumaliza tatizo la kukosa choo kwa haraka

Tatizo la kukosa choo ni moja ya matatizo ambalo huweza kumkuta mtu yoyote katika maisha yake bila kujali umri.

Hili ni miongoni mwa matatizo ambayo huweza pia kukufanya kukosa raha kwani hata pale unapopata choo huambatana na maumivu makali wakati wa zoezi hilo.

Kuna sababu mbalimbali ambazo huweza kuchangia tatizo hili miongoni mwa sababu hizo ni pamoja na kukosa vyakula vyenye nyuzinyuzi za kutosha yaani 'fiber' lakini pia hata kutokunywa maji ya kutosha nayo huchangia tatizo hili.

Kingine ambacho pia huweza kuchangia tatizo hili na watu wengi hawakifahamu ni pamoja kutofanya mazoezi ya mwili au kusongwa na msongo wa mawazo.

Miongoni mwa vitu unavyoweza kutumia ili kupunguza tatizo hili ni pamoja na hivi vifuatavyo;-

Mafuta ya samaki ambayo yamesheheni kirutubisho cha omega 3 ambayo husaidia kurekebisha umeng'enyaji wa chakula ndani ya mwili.

Mafuta ya mzaituni nayo yanaweza kuwa moja ya njia ya kupunguza tatizo hili la kukosa choo. Maafuta haya huenda kuamsha mfumo wa umeng'enyaji chakula tumboni na hivyo kusaidia kuepuka tatizo hilo.

Juisi ya limao nayo huweza kutumika kwa kupunguza tatizo hili, juisu ya limao husaidia kusafisha sumu kwenye utumbo mpana na hivyo kupunguza uwezekano wa tatizo hilo. Ni vizuri juisi hii ikachanganywa na maji ya uvuguvugu kwa matokeo mazuri zaidi.

Kufanya mazoezi na kupunguza msongo wa mawazo pia ni muhimu ili kupunguza uwezekano wa kukumbwa na tatizo hili.

Kwa ushauri zaidi wasiliana nasi kwa simu namba +255 716 300 200, +255 769 400 800, +255 784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment