Friday, 26 May 2017

Njia 5 asili za kuzuia kutapika

6 Effective Home Remedies to Prevent Vomiting
Unapokula chakula mara zote huwa unatarajia kufurahia chakula na si kupata karaha, lakini kuna wakati chakula huweza kuwa kikwazo hasa pale unapokula na kupata kichefuchefu na hatimaye kutapika.

Kutapika hutokana na tatizo ndani ya mfumo wa uyeyushaji wa chakula (digestive system). Kichefuchefu na kutapika mara nyingi huwa na uhusiano na mfumo wa uyeyushaji wa chakula ndani ya tumbo.

Iwapo kutapika kutakuwa kumesababishwa na mzio wa chakula, kula kuzidi kiasi au sumu ndani ya chakula, ni vyema kutapika kuendelee badala ya kuzuia ili chakula chote kilicho tumboni kitoke kwani baada ya kutapika hali itarudi kuwa ya kawaida.

Sasa pale endapo utaona kuna umuhimu au haja ya kuzuia kutapika ili kukinga athari kubwa zinazoweza kujitokeza baadaye ikiwa ni pamoja na kupungukiwa maji mwilini

Unaweza kutumia njia hizi tano za kuzuia kutapika

1. Juisi ya chungwa
Hii inatakiwa iwe juisi halisi kabisa iliyoandaliwa nyumbani na sio zile za viwandani. juisi hii husaidia kurejesha haraka vitamini na virutubisho vilivyopotea ndani ya mwili baada ya kutapika

2. Maji ya limao
Vitamini pamoja na madini yalipo ndani ya limao husaidia kuzuia kutapika kwa haraka

3. Mchanganyiko wa maji ya sukari na chumvi
Mchanganyiko huu humsaidia mhusika anayetapika kurudisha hali ya unyevunyevu ndani ya mwili na husaidia kuzuia mwili kukosa nguvu

4. Karafuu
Weka vipande kadhaa vya karafuu mdomoni na utafune kwa mda, hii itakusaidia kuzuia kutapika kwa haraka

5. Tangawizi
Saga tangawizi kisha weka kwenye maji  ongeza na kijiko kimoja cha asali kisha utakunywa mchanganyiko huo ili kuzuia hali ya kutapika.

Zingatia
Ni vyema kuwasiliana nasi kwa ufafanuzi zaidi wa njia hizi tupigie kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment