Friday, 19 May 2017

Njia asili ya kumsaidia mtu aliyeteguka

Habari za leo mpendwa msomaji wetu wa www.dkmandai.com karibu katika muendelezo wetu wakufahamishana mambo mbalimbali kuhusu tiba asilia na mimea mbalimbali kwa ujumla.

Leo nimeona ni vyema tujuzane kuhusu hii mbinu ya asili inayoweza kukusaidia pale unapopata uvimbe kutokana na kuumia, kuteguka au kushtuka.

Inawezekana umewahi kuumia au mtoto wako amewahi kuteguka kutokana na michezo na ukajikuta akipata uvimbe , lakini ukashindwa ni mbinu gani utumie ili kupunguza uvimbe ukiwa bado nyumbani kwako.

Sasa leo kuna hii njia unayoweza kuitumia na ikakusaidia sana kuondosha uvimbe wa sehemu iliyotokana na kuumia kwa kuteguka au kushituka unachopaswa kuwa nacho ni ukwaju pamoja na chumvi tu, ili kukamirisha tiba hii.

Kamua ukwaju ili kupata juisi yake nzito, kisha ongeza chumvi nyingi na ukoroge vizuri kisha mchanganyiko wako huo ukishachanganyika vizuri utautumia kwa kupaka sehemu zote zenye uvimbe uliotokana na kuumia au kuteguka.

Baada ya kupaka, utaacha mchanganyiko huo hapo hapo. Baada ya saa 12 paka tena, endelea hivyo hivyo hadi pale utakapoona uvimbe utakapokuwa umepungua kiasi cha kutosha au kuwa katika hali ya kawaida.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com


Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment