Monday, 15 May 2017

Ramadhani hiyo inakuja, karibu tuvijue vinywaji muhimu kwa wakati huo

Assalam Aleykum msomaji wangu wa www.dkmandai.com tukiwa karibu tunaingia kwenye mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani leo nimeona tufahamishane namna ya kuzuia kiu wakati wa kipindi hicho cha mfungo.

Wakati wa kipindi hiki wafungaji wanashauriwa katika kipindi cha saa moja baada ya kufuturu hadi nusu saa kabla ya wakati wa daku kunywa maji bilauri 8, huku wakiendelea kula vyakula vyenye ufumwele vinavyosaidia kuzuia kiu kwa muda mrefu.

Wafungaji pia wanashauriwa kujiepusha kunywa chai, kahawa au soda kwani vinywaji hivyo vina kiwango cha juu cha kafeini inayoufanya mwili upoteze maji kwa haraka na hivyo mhusika kuhisi kiu zaidi.

Aidha, wafungaji wanapaswa kutambua kuwa, unywaji wa maji mengi wakati wa daku husaidia kuzuia kuhisika kiu baadaye.

Pamoja na hayo, ulaji wa matunda yenye majimaji kabla ya kufungu ni vizuri kwani husaidia kutohisi kiu baadaye wakati wa mfungo.


Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu namba +255 716 300 200/ +255 769 400 800/ +255 784 300 300 au Barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment