Tuesday, 2 May 2017

Tangawizi na karoti zikichanganywa unapata faida hizi 5


Juisi za matunda ni moja ya kati ya vitu muhimu ambavyo huhitajika katika kujenga afya za miili yetu hususani unapopata juisi za matunda asilia kabisa.

Leo nimeona ni vyema tuzungumzie kuhusu juisi ya karoti iliyochanganywa na tangawizi kiasi.

Juisi hii ya karoti na mchanganyiko wa tangawizi inafaida mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusheheni virutubisho lukuki.

Juisi ya karoti na mchanganyiko wa tangawizi huupatia mwili vitamin A, K, ambazo kwa pamoja husaidia kulinda afya ya kucha, mifupa pamoja na nywele zetu.

Uwepo wa tangawizi ndani ya juisi hii umekuwa ukiifanya juisi hii kuwa suluhisho la matatizo ya kukatika kwa nywele na kuzifanya kuwa imara zaidi.Hivyo ni juisi nzuri kwa wanawake wanaopenda urembo wa nywele.

Juisi hii pia inaelezwa kuwa na uwezo wa kukinga dhidi ya saratani, matumizi ya juisi ya karoti yenye mchanganyiko wa tangawizi husaidia kuukinda mwili dhidi ya matatizo ya saratani za aina mbalimbali kwani husaidia kuua seli zinazoweza kuchangia matatizo hayo.

Aidha, juisi hii husaidia kuimarisha kinga za mwili, kutokana na kuwa na vitamin A ndani yake hivyo kumfanya mhusika kutozongwa na magonjwa ya mara kwa mara.

Mbali na hayo pia juisi hii husaidia kulinda meno na fizi, karoti pekee yake kwanza inatosha kwa kuwa mlinzi mzuri wa kinywa, hivyo matumizi ya glasi moja ya juisi ya karoti iliyochanganywa na tangawizi baada ya kula husaidia sana kulinda afya ya kinywa kwa ujumla.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment