Saturday, 27 May 2017

Tatizo moja la kiafya ambalo huweza kusaidiwa na maziwa mtindi

Tatizo la tumbo kujaa gesi ni moja ya tatizo ambalo huwasumbua wengi na kusababisha maumivu ya tumbo au tumbo kuwa na miungurumo ya hapa na pale.


Tatizo hili huchangiwa sana na aina ya vyakula unavyokula hususani vile vyenye mafuta mengi, lakini pia husababishwa na vinjwaji unavyokunywa hasa soda au bia.


Kwa kawaida aina ya vyakula hivyo vinapoingia tumboni, huwa na tabia ya kuchelewesha usagaji wa chakul, hivyo huleta matatizo kwenye mfumo mzima wa usagaji chakula.


Maziwa ya mtindi huweza kuwa suluhisho la tatizo hili na ni vizuri ukatumika ule mtindi halisi, maziwa hayo husaidia sana kurekebisha mfumo wa usagaji wa chakula na kuufanya kuwa mwepesi.


Pia papai husaida sana tatizo hili kwa sababu tunda hilo huenda kurekebisha mfumo wa usagaji wa chakula na uwezo huo hutokana na uwepo wa kirutubisho cha ‘enzyme’ ambacho hupatikana ndani ya papai.

Zingatia
Kama ungependa kutuuliza maswali zaidi kuhusu mada hii na hata masuala mengine mengi kuhusu mimea tiba, matunda na lishe bora kwa ujumla wake basi tupigie sasa kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment