Monday, 1 May 2017

Unga wa ngano humaliza tatizo la mdudu wa kidole (whitlow)

Je, ni mara ngapi umesikia kuhusu tatizo la mdudu wa kidole? Huenda na wewe inawezekana umewahi kpatwa na tatizo hili.

Tatizo hili hutokea kama aina ya jipu kwenye ncha ya kidole chochote cha mkono hasa chini ya ukucha.

Tatizo hili huchangia maumivu makali na kuleta usumbufu wa muda mrefu, lakini huweza kupata ufumbuzi kwa njia hii.

Sasa basi kama unasumbuliwa na tatizo hilo unaweza kutumia njia hii asili ili kumaliza tatizo hilo kwa haraka.

Chukua unga wa ngano kidogo, kisha ongeza maji kidogo na uchanganye kwa pamoja hadi ionekane kama tui la nazi.

Baada ya hapo ongeza kiasi kidogo cha sukari pamoja na matone kumi na tano ya mafuta nyonyo, harafu koroga kwa pamoja na pasha moto

Mara baada ya hatua hizo utachukua mchanganyiko huo , paka kwa wingi kwenye kitambaa kisafi kisha funga kidole kilichoathirika kwa kitambaa hicho.

Rudia tiba hiyo mara mbili kwa siku asubuhi na jioni kwa muda wa siku tano.

Kwa maelezo zaidi au ufafanuzi mpigie Mtaalam Mandai kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment