Tuesday, 6 June 2017

Aina 2 ya matunda yenye uwezo wa kupunguza maumivu ya viungo


Maumivu ya mishipa au gout yanaweza kuleta maumivu makubwa katika maungio hasa katika kidole gumba cha mguu.

Lakini pia unaweza pia kujisikia maumivu katika kifundo cha mguu, magotini au katika maungio mengine ya mwili.

Ikiwa unasikia maumivu kila mara katika mikono, vidole, magoti, katika maungio mbalimbali mwilini unashauriwa ukapate vipimo zaidi.

Yafuatayo ni baadhi ya matunda ambayo huweza kupunguza tatizo la maumivu mbalimbali ya mwili:-

1. Zabibu
Zabibu zina kiasi kingi cha kiuaji sumu na zinaweza kupunguza maumivu ya gout kwa haraka zaidi. Mbegu za tunda la zabibu zina kitu mhimu kiitwacho phenomenology ambacho ni kiuaji sumu kingine kinachosaidia kupigana na aina zote za maumivu ya mishipa ikiwemo gout. Hivyo unashauriwa kutumia tunda hili mara kwa mara ili kuepuka tatizo hili.


2. Nanasi
Nanasi lina kimeng’enya mhimu kiitwacho ‘bromelain’ ambacho kina sifa ya kuzuia muwako wa ndani ya mwili (inflammation). Kwahiyo mhusika wa tatizo hili anapotumia tunda kila siku huweza kusaidia kupunguza maumivu yatokanayo na gout.

Kwa ufafanuzi zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore ya simu yako kisha tafuta Mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment