Wednesday, 28 June 2017

Aina 4 ya mazoezi yenye kupunguza ukubwa wa kifua kwa mwanamke


Wanawake hukwazika pale wanapokuwa na vifua vikubwa (matiti) na wengi hujikuta wakitumia dawa mbalimbali ambazo kuna wakati huweza kuwasababishia madhara.


Leo nimeona nikueleze msomaji wangu baadhi ya mazoezi ambayo mwanamke akiyafanya huweza kumsaidia kupunguza ukubwa wa kifua chake.

1. Kupanda ngazi na kushuka 
Climbing The Stairs
Unaweza kufanya mazoezi ya kupanda na kushuka kwenye ngazi huku ukikimbia kwa taratibu ndani ya dakika kumi na tano hadi ishirini. Zoezi hili husaidia kupunguza ukubwa wa kifua kwa mwanamke unaweza kufanya kwa mwezi mfululizo hadi miezi mitatu.

2. Kuogelea.

Hili nalo ni zoezi nzuri kwa mwanamke anayehitaji kupunguza ukubwa wa kifua, hii huweza kusaidia endapo litafanyika mara kwa mara.

3. Kukimbia

Zoezi hili la kukimbia nalo huweza kusaidia kupunguza ukubwa wa kifua kwa mwanamke na inapaswa kufanya zoezi hili angalau kwa dakika 20 kila siku.

4. Push Up
Push Ups
Mazoezi ya push up nayo huweza kusaidia kupunguza ukubwa wa kifua unaweza piga angalau mara 5 kwa siku na itakusaidia.

Unaweza kuuliza maswali mbalimbali kwa kupiga simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.


No comments:

Post a Comment