Tuesday, 13 June 2017

Aina 4 ya vyakula rafiki kwa wenye matatizo ya moyo


Unaambiwa kuwa uzuri wa tatizo ni pale unapolijua kuliko kutolijua na siku zote hakuna jambo jema kama mtu mwenye matatizo ya kiafya kujua ni aina gani ya mlo anaopaswa kula au kutokula.

Baadhi ya magonjwa kama vile ‘presha’, vidonda vya tumbo, magonjwa ya moyo, n.k, mara nyingi huhitaji kubadili hata mtindo wa maisha hususani mpangilio wa vyakula.

Leo tutaangalia baadhi ya vyakula na matunda anavyopaswa kula mtu mwenye ugonjwa wa moyo, ambavyo huweza ama kudhibiti hali yake isiendelee kuwa mbaya zaidi

1. Zabibu.
Zabibu ni tunda linaloongoza kwa ubora linapokuja suala la kuimarisha afya ya moyo. Ili kupata matokeo mazuri, andaa ratiba maalum ya kula zabibu peke yake kwa siku kadhaa mfululizo, juisi ya zabibu pia hufaa zaidi.

2. Apple 
Tunda hili husaidia kwa mgonjwa wa moyo, hasa wenye matatizo ya kuwa na moyo dhaifu, hivyo wale wenye matatizo hayo wanashauriwa kupendelea kula apple mara kwa mara, ikiwemo juisi yake ambayo huweza kuleta matokeo mazuri zaidi.

3. Kitunguu maji
Kitunguu kina faida kubwa kwa mgonjwa wa moyo, kwakuwa huweza kurekebisha mafuta ya kolestro ndani ya mwilini na kuuweka mwili katika hali yake ya kawaida. Kwa matokeo mazuri, kunywa kijiko kimoja (cha chakula) cha juisi ya kitunguu.

4.Asali
Asali ina virutubisho ambavyo vina uwezo wa kuzuia aina zote za matatizo ya moyo. Inaelezwa kwamba asali inaboresha mzunguko wa damu mwilini, halikadhalika inaondoa matatizo mengine ya moyo. Kijiko kimoja (cha chakula) cha asali kikitumiwa kila siku mara baada ya mlo, kina uwezo wa kutoa kinga dhidi ya maradhi yote ya mwili.

Pamoja na hayo, matunda na mbogamboga kwa ujumla wake, ndiyo vyakula muhimu kwa magonjwa mengi ya moyo, vyakula hivyo vina uwezo wa kudhibiti ugonjwa huo na kuimarisha moyo.

Sambamba na hayo, watu wenye matatizo ya moyo hushauriwa kuepuka matumizi ya chumvi nyingi, kahawa, sukari, sigara nk. Hayo yakizingatiwa, mgonjwa anaweza kuishi na tatizo la moyo bila kusumbuliwa.

Zingatia
Kwa ushauri zaidi ni vyema kufika hospitali iliyokaribu nawe kwa msaada wa kitaalam zaidi.

Pia unaweza kutupigia kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment