Wednesday, 7 June 2017

Aina 5 za matunda, mbogamboga na viungo vyenye kusafisha mishipa yako ya damu


Ndani ya miili yetu kuna mishipa ya damu ambayo kazi yake kubwa ni kusambaza hewa ya oxygen pamoja na virutubisho mbalimbali ndani ya mwili.

Lakini inapotokea mishipa hiyo ya damu ikazongwa na vitu mbalimbali hususani cholesterol huweza kuchangia mzunguko wa damu kuwa hafifu mwilini na hata kusababisha matatizo kadhaa ya kiafya.

Matatizo ya kuzongwa na cholesterol kwa  mishipa ya damu kimsingi huchangiwa na mtindo wa maisha wa mhusika hasa ulaji.

Hivyo leo nimeona nikwambie msomaji wangu baadhi ya vyakula, mboga, matunda na viungo ambavyo ukivitumia vitakwenda kusaidia kusafisha mishipa yako ya damu.

1. Juisi ya Komamanga
Juisi ya tunda hili huenda kuamsha uzalisha ndani ya mwili wa kitu kiitwacho nitric oxide, ambayo huenda kusaidia kufungua mishipa ya damu mwilini. Unachohitajika kufanya ni kuhakikisha unapata glasi moja au mbili za juisi hiyo kila siku au tunda lenyewe.

2. Parachichi
Tunda hili husifika kwa kuwa na vitamin E ambayo husaidia kupunguza cholesterol mwilini pamoja na hayo ndani ya tunda hili kuna mafuta mazuri kwa mwili ya  monounsaturated fatty acids ambayo husaidia kulinda matatizo kama hayo.

3. Spinach
Hii ni aina ya mboga ya majani yenye kiasi kikubwa cha vitamin A, C ambazo husaidia kuzuia cholesterol ndani ya kuta za mishipa ya damu mwilini.

Pia mboga hii inakiwango kizuri cha madini ya potassium pamoja na folic ambayo nayo husaidia kupambana na kiwango cha cholesterol mwilini.

4. Kitunguu swaumu
Ni kiungo chenye uwezo wa kuzuia mishipa ya damu kuzongwa na uchafu mbalimbali mwilini utokanao na vyakula tunavyokula kutokana na kiungo hiki kuwa na utajiri wa kitu kiitwacho  antioxidants.

Zingatia
Kitunguu swaumu si kuzuri kwa matumizi ya mama mjamzito, au anayenyonyesha, watoto na watu wenye presha ya kupanda. Hivyo ni vyema kabla ya kutumia ukawasiliana na wataalam wa mimea na lishe, au tiba asili.

5. Apple au tofaa
Ni tunda ambalo pia husaidia kusafisha mishipa ya damu kutokana na kuwa na kiwango kizuri cha nyuzinyuzi (fiber) ziitwazo 'pectin' ambazo huweza kufanya kazi ya kusafisha cholesterol mwilini.

Kwa ufafanuzi zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore ya simu yako kisha tafuta Mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment