Tuesday, 20 June 2017

Aina za vyakula vinavyoweza kujenga au kubomoa afya ya mtoto wako

Watoto ili wawe na afya bora wanahitaji umakini mkubwa sana hasa katika aina ya vyakula wanavyoandaliwa.

Chakula bora kwa watoto ni pamoja na vyakula tofauti tofauti ambavyo mtoto anahitaji kupata kila siku, ikiwa ni  pamoja na matunda, mboga maziwa na aina yeyote ya vyakula vyenye asili ya nyama, samaki na maharagwe (nafaka).

Mzazi anatakiwa kuhakikisha anapunguza kiasi cha sukari kwenye vinywaji vya watoto na ulaji wa peremende kwa watoto.

Pia mzazi huhitajika kupunguza kiasi cha chakula ambacho hupikwa kwa mafuta ya kuchemka kama vile keki, viazi 'chips', vitumbua, kababu, sambusa, chapati, soseji, biskuti na vyakula vyote vya kutumbukizwa kwenye mafuta.

Kumbuka
Maziwa ni muhimu sana kwa utengenezaji wa meno na mifupa ambayo yenye nguvu, lakini pia ulaji wa chakula bora husaidia watoto kuwa na afya bora, kuwa na nguvu, kufanya vyema hata katika masomo yao na kupunguza uzito usiohitajika.

Unaweza pia kupokea ushauri wa bure kutoka kwetu kuhusu masuala ya lishe bora tupigie sasa kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com tupo kwaajili yako karibu.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment