Wednesday, 14 June 2017

Dalili 5 ambazo mwanamke hupaswi kuzipuuza zinapojitokeza mwilini mwako


Picha kwa hisani ya mtandao
Afya za wanawake au kinamama ni moja ya mambo ambayo pia hupaswa kupatiwa kipaumbele zaidi katika maisha.

Leo naomba nikueleze msomaji wangu dalili ambazo mwanamke haupaswi kuzipuuza mara unapoziona.

1. Kuhisi maumivu makali kifuani
Kamwe mwanamke hutakiwi kupuuza mara yanapojitokeza maumivu ya aina hiyo unachotakiwa kufanya ni kufika hospitali kwa uchunguzi zaidi.

2. Matiti kuvimba
Ukiona mabadiliko ya matiti yako ikiwa ni pamoja kuvimba bila sababu za msingi ni vyema kuwaona wataalam wa afya, lakini kumbuka kuwa hali hiyo pia kunawakati huweza kuchangiwa na aina ya sidiria uliyovaa hasa inapokuwa mpya na yenye kubana sana.

3. Kuona siku zako  mara baada ya kukomaa kwa hedhi
Mwanamke unapoona hali hii pia unatakiwa kupata ushauri wa wataalama wa afya ili kujua undani wa hali hiyo.

4. Miguu kuvimba
Miguu kuvimba huweza kuashiria tatizo kwa kinamama, hivyo mwanamke usikae kimya mara unapoona mabadiliko hayo ya miguu ikiwa ni pamoja na miguu kuvimba.

5. Maumivu ya kichwa ya mara kwa mara
Unapohisi maumivu ya kichwa kila siku au mara kwa mara tambua kuwa hiyo nayo si dalili nzuri katika afya yako pia na hivyo unapaswa kuwaona wataalam wa afya kwa ushauri zaidi.

Kwa msaada zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment