Friday, 9 June 2017

Dalili 6 ambazo hupaswi kuzipuuza mara unapoziona kwa mtoto

Picha kwa msaada wa mtandao
Watoto siku zote huhitaji uangalizi wa karibu kila wakati na umakini mkubwa sana katika kuhakikisha wanakuwa salama wakati wote.

Kwa sasa familia nyingi zimekuwa zikiwatumia kinadada wa kazi katika kuwatunza watoto kutokana na wazazi kukimbizana na shughuli za kimaisha hasa za kutafuta fedha.

Pamoja na hayo, leo nimeona nikueleze msomaji wangu dalili 6 ambazo hupaswi kuzipuuza mara tu unapoziona kwa mtoto.

1. Kupumua kwa shida
Mtoto anapokuwa katika hali hiyo ghafla ni vyema kuchukua hatua kwani huweza kuwa ni dalili za matatizo fulanifulani ikiwa ni pamoja na pumu, kwahiyo ni vyema kumuwahisha mara moja mtoto hospitali unapoona dalili hizo.

2. Mtoto kubanwa na kiu sana
Unapoona kila mara mtoto wako anahitaji kunywa maji ni vyema kwenda kumuona daktari kwa uchunguzi zaidi kwani huweza kuwa dalili za kisukari wakati mwingine (diabetes type 1).

3. Maumivu wakati wa haja ndogo (kukojoa)
Mtoto ukiona anapatwa na maumivu wakati wa haja ndogo inaweza kuwa ni dalili za matatizo ya UTI . Hivyo unashauriwa kuwaona wataalam wa afya mara unapoona tatizo hilo kwa mtoto.

4. Uchovu uliopitiliza
Kuna wakati unaweza kukuta mtoto wako amekuwa mchovu na hachezi hata na wenzake kabisa na wala hacheki, usikae kimya uonapo hali hiyo hakikisha unaenda hospitali kwa uchunguzi zaidi kwani huweza kuwa ni dalili za matatizo fulani ya kiafya.

5. Kutapika 
Mtoto anapotapika nayo si dalili nzuri kwa mtoto huashiria kuna shida hivyo hupaswi kukaa bila kwenda kuwaona wataalam hospitali kwa uchunguzi zaidi wa mtoto wako.

6. Joto kali la mwili
Hii nayo si ishara njema kwa mtoto na huashiria uwepo wa tatizo kwenye afya ya mwanao , hivyo unapoona joto la mtoto limepanda usikae kimya fika mara moja kwenye hospitali iliyokaribu nawe kwa ushauri zaidi

Kwa sasa naomba niishie hapo msomaji wangu kumbuka kuwa siku nzote mtoto anahitaji uangalizi wa hali ya juu muda wote.

Kwa maelezo na ufafanuzi zaidi tupigie kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore ya simu yako kisha tafuta Mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment