Saturday, 17 June 2017

Dalili hizi 5 ukiziona kwako usipuuze nenda hospitali haraka


Kila utofauti unaojitokeza mwilini mwako au katika afya yako kamwe usipuuze kwani huwa na maana yake.

Hivyo leo naomba nikwambie hizi ishara 5 ambazo zikijitokeza kwako kamwe usikae kimya ni lazima uonane na wataalam wa afya mara moja na haraka iwezekanavyo.

1. Udhaifu katika mikono yako na miguu
Hii si dalili ya kuipuuza hata kidogo kwani huweza kuwa ni moja ya kiashiria cha kiharusi au 'stroke' hasa pale dalili hiyo inapoonekana upande mmoja wa mwili.

2. Maumivu sehemu ya kifua
Haya nayo si aina ya maumivu ya kuyapuuza kwani huweza kuwa ni dalili za magonjwa ya moyo, mshtuko wa moyo, hivyo unapohisi maumivu ya aina hiyo jitahidi kufika hospitali iliyokaribu nawe na kuwaona wataalam wa afya.

3. Uonapo damu kwenye haja ndogo(mkojo) yako
Kama kuna damu kwenye haja ndogo yako na unapatwa na maumivu makali hasa ya mgongo hiyo huweza kuwa dalili ya mawe kwenye figo hivyo ni vyema kwenda hospitali kwa uchunguzi zaidi.

4. Mapigo ya moyo kubadilika 
Inawezekana mapigo yako ya moyo yakawa yakienda kasi zaidi kuliko ilivyo kawaidia usinyamaze kimya waone wataalam kwa ushauri zaidi.

5. Unapozongwa na mawazo ya kujiua
Hii nayo si dalili njema katika maisha yako unapoona hali hiyo unaweza omba ushauri kwa wataalam wa saikolojia au kuwashirikisha ndugu au jamaa zako wa karibu ili kupata ushauri mzuri zaidi.

Unaweza pia kupokea ushauri wa bure kutoka kwetu kuhusu masuala ya lishe bora tupigie sasa kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com tupo kwaajili yako karibu.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment