Saturday, 17 June 2017

Dalili za awali kuwa mwili wako haupo sawa kiafya


Kwa kawaida sisi miili yetu binadamu huonesha dalili fulani endapo kuna tatizo ndani ya mwili, lakini kwa bahati mbaya sana watu wengi hawana uelewa wa dalili hizo.

Leo naomba nikueleze hizi dalili chache ambazo huashiria uwepo wa tatizo ndani ya mwili.

Midomo kuwa mikavu
Midomo ni sehemu tosha ya kuashiria tatizo ndani ya mwili na mara nyingi huweza kuashiria kupungua kwa kiwango cha maji mwilini. Kwani unapokosa maji ya kutosha mwilini basi hata midomo nayo huanza kupoteza unyevunyevu. Hivyo kwa wale wakinadada ambao hulazimika kulainisha midomo yao kwa 'lips shine' basi watambue kuwa wana upungufu wa maji mwilini.

Ili kukabiliana na tatizo hili unapaswa kuanza kunywa maji ya kutosha zaidi ilivyo sasa angalau glasi 8 kwa siku

Kufunga choo

Hii huwa ni dalili ya wazi kuwa mhusika anashida ya ukosefu wa kamba lishe (fibre) mwilini. Kwa kawaida binadamu anatakiwa kupata choo kikubwa kila siku kilicho laini na kingi. Iwapo hupati choo kila siku na ukipata unapata kigumu, tena kidogo, jua una matatizo!

Haja kubwa ni muhimu kwa sababu ndiyo inayosafisha tumbo, uchafu unapokaa tumboni kwa muda mrefu, sumu zilizomo kwenye haja kubwa hurejea mwilini na kusababisha madhara mengi ya kiafya.

Vidonda vya mdomo

Vidonda vya midomoni, huwa ni dalili moja wapo ya dalili za upungufu wa vitamini B mwilini na mara nyingi huwatokea wale wapenzi wa kula vyakula vya kwenye makopo (processed foods) na kula sukari kwa wingi.

Njia pekee ya kuondokana na tatizo hili ni kuanza kula vyakula vyenye kuongeza vitamin B kwa wingi. Miongoni mwa vyakula vyenye kiwango kingi cha vitamin B ni pamoja na viazi vitamu na nafaka isiyokobolewa nk.

Kwa maelezo zaidi kuhusu mada hii na mengine mengi tutafute kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment