Thursday, 29 June 2017

Fahamu namna ganda la ndizi linavyoweza kumaliza tatizo la chunusi

Cut The Banana Peel
Uso kuwa na chunusi ni moja ya mambo ambayo huwakwaza wengi wenye shida hiyo na kuwafanya hata kutojiamini wanapokuwa mbele za watu.

Mara nyingi tatizo hili huwakumba vijana wengi hasa katika hatua za ukuaji wao, lakini leo nimeona nikueleze hii mbinu nyingine ambayo huenda itaweza kukusaidia kupunguza tatizo hilo au kupunguza madhara yake.


Nataka nikwambie kuhusu ganda la ndizi, najua wengi tunaifahamu ndizi kama tunda lakini si wote tunafahamu kama ganda la tunda hilo linaweza kutumika kwa matatizo mengine likiwemo hili la kuwasaidia wenye chunusi.

Unachopaswa kufanya ni kupata ndizi iliyoiva na kuiosha vyema kisha menye ganda hilo kwanza na kuliweka sehemu safi wakati huo anza kwanza kwa kusafisha uso wako kwa maji yenye uvuguvugu.

Baada ya hatua hiyo utachukua ganda lako la ndizi na kusugua kwa taratibu sana sehemu iliyoathirika (yenye chunusi) au madoa ya chunusi kwa dakika 2 hadi 3.
Rub The Peel


Mara baada ya hatua hiyo acha kwa dakika kumi uso wako ukiwa hivyo hivyo, kabla ya kunawa na zikipita dakika 10 unaweza kuosha uso wako. Rudia zoezi hilo kila siku asubuhi na jioni kwa muda wa wiki 3 hadi 4.

Kwa maelezo na ufafanuzi zaidi unaweza kuwasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.
No comments:

Post a Comment