Thursday, 8 June 2017

Fahamu namna kitunguu swaumu kinavyoweza kuokoa ndoa yako

Ndoa nyingi zinapopatwa na changamoto ya kutopata mtoto lawama nyingi huelekezwa kwa kinamama zaidi bila kujali kuwa tatizo hilo kunawakati huweza kuwa upande wa mwanaume.

Miongoni mwa sababu ambazo huchangia tatizo la ugumba kwa wanaume ni pamoja na kukaa sehemu sehemu yenye joto kali sana kwa muda mrefu au kufanya kazi kwenye mazingira yenye kemikali zinazoathiri uzalishaji wa mbegu za kiume kwa kipindi kirefu.

Sababu nyingine ni tabia ya unywaji pombe kupindukia na uvutaji wa sigara sambamba na matumizi ya dawa za kulevya kama kokeni, bangi jambo ambalo hupunguza idadi na kiwango (quality) cha manii (shahawa) .

Tatizo hili pia huweza kuchangiwa na kukosekana kwa baadhi ya vichocheo mwilini madhara yatokanayo na magonjwa ya korodani au kwenye mishipa ya korodani.

Magonjwa mengine ambayo huweza kuchangia mwanaume kuwa na tatizo la uzazi ni pamoja na kuzongwa na magonjwa ya ngono kwa muda mrefu pamoja msongo wa mawazo.

Sasa leo nimeona nikwambie kuhusu hiki kiungo kiitwacho kitunguu swaumu jinsi kinavyoweza kumsaidia mwanaume mwenye tatizo la ugumba au kutotungisha mimba.

Jinsi ya kukitumia
Hakikisha kila siku unapata kiasi fulani cha kitunguu swaumu kwenye mlo wako, hivyo unaweza kukisaga kisha kuweka kwenye mboga unazokula karibu kila siku. Hii huenda kusaidia kuzipa uwezo na nguvu mbegu zako za kuweza kurutubisha yai la mwanamke na hatimaye kusababisha ujauzito.

Kwa maelezo na ufafanuzi zaidi tupigie kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore ya simu yako kisha tafuta Mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment