Thursday, 29 June 2017

Faida 3 za tikitimaji kwa watu wenye kisukari


Kama utakuwa ni mfuatiliaji mzuri wa tovuti yetu hii naamini kuwa utakuwa unafahamu kuwa tumeshazungumza sana kuhusu matatizo  ya kisukari.

Mara kadhaa tumeshazungumza kuhusu dalili zake chanzo na namna ya kukabiliana na tatizo hili na hata baadhi ya makundi ya vyakula yanayofaa.

Leo si mbaya tukiangalia msaada wa tunda la tikitiki maji kwa watu wenye shida ya kisukari.

1. Hufaa kwa afya ya macho.
Mara nyingi watu wenye kisukari baadaye huanza kupoteza uwezo wao wa kuona vizuri na wengine kutoona kabisa. Hivyo kutokana na tikitimaji kuwa ni chanzo kizuri cha vitamin A ambayo ni muhimu sana kwa afya ya macho.

2. Hulinda afya ya figo
Matatizo ya figo ni moja ya mambo ambayo huwazonga pia watu wenye shida ya kisukari, lakini tikitimaji linaweza kutoa ahueni kwa tatizo hilo kutokana na tunda hilo kuwa na uwezo wa kulinda afya ya figo. 

Tunda la tikitimaji huweza kuipunguzia figo majukumu yake kutokana na kuwa na madini ya potassium ambayo husaidia kushusha kiwango cha uric acid ndani ya damu.

3. Husaidia kurekebisha mm'engenyo wa chakula
Watu wenye kisukari pia husumbuliwa na tatizo la kuwa na mmen'genyo mbovu wa chakula, lakini watu wenye shida hiyo wanapotumia tikitimaji huweza kuwasaidia kutokana na tunda hilo kuwa na wingi wa maji maji pamoja na nyuzinyuzi 'fiber'.

Unaweza kuuliza maswali mbalimbali kwa kupiga simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment