Wednesday, 21 June 2017

Faida 4 za parachichi kwa wanawake


Parachichi ni miongoni mwa matunda mazuri yenye ladha pia ambayo hupatikana kwa wingi hapa nchini Tanzania.

Leo naomba nikueleze msomaji wangu kuhusu faida za tunda hili hasa kwa wanawake.

1.Imesheheni vitamin B6 
Hii humsaidia mwanamke katika kuimarisha afya yake hasa afya ya akili au ubongo zaidi pamoja na kuongeza uwezo wa ubongo pia.

2. Tunda lenye madini ya calcium na vitamin
Ambazo ni muhimu pia kwa mawanamke kutokana na kusaidia kuwa na mifupa imara kwa mwanamke. Pia ulaji wa tunda hili husaidia kuongeza vitamin mbalimbali mwilini pamoja na madini.

3. Magnesium
Haya ni miongoni mwa madini yanayopatikana kwenye parachichi na husaidia kuimarisha kinga za mwili za mwanamke , lakini mbali na hayo, madini haya pia husaidia kujenga afya ya mifupa.


4. Hupunguza maumivu ya viungo.
Parachichi linapotumiwa mara kwa mara huweza kusaidia kupunguza maumivu ya hapa na pale ya viungo

Unaweza pia kupokea ushauri wa bure kutoka kwetu kuhusu masuala ya lishe bora tupigie sasa kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com tupo kwaajili yako karibu.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment