Monday, 19 June 2017

Faida za kiungo cha kotimiri


Kotimiri ni aina ya mmea ambao majani yake na mbegu zake huweza kutumika kama kiungo katika vyakula.

Naamini kwamba wengi wetu pengine hatufahamu kuhusu mmea huu au huenda ikawa ni mara yako ya kwanza kusikia kiungo hiki kinachoitwa Kotimiri.

Majani ya kotimiri yamekuwa yakiaminika kwa kusaidia kupunguza matatizo ya msokoto wa tumbo ambao mara nyingine huweza nyingi kuchangia mtu kuharisha.


Aidha, kiungo hiki ni kizuri sana kwa wale wenye shida ya kukosa hamu ya kula. Hii ni kutokana na kuwa na uwezo mkubwa wa kuchochea vimeng’e nyo tumboni na hivyo kuongeza hali ya kuhisi njaa.

Endapo unawaza ni wapi unaweza kukipata kiungo hiki basi, jaribu kutembelea masoko mbalimbali hapa nchini, lakini pia kiungo hiki hupendelewa sana kutumiwa na wahindi.

Unaweza kuwasiliana nasi kwa mawasiliana yafuatayo: 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300 Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment