Friday, 9 June 2017

Hatari ya matumizi ya chumvi, fahamu njia ya kuepuka matumizi ya chumvi


Miili yetu inahitaji chumvi kwa kiasi kidogo sana kwasababu chumvi huupatia mwili madini ya Sodium ambayo huhitajika kusafirisha taarifa za mfumo wa fahamu n.k.

Matumizi ya chumvi nyingi huongeza uwezekano wa kupata shinikizo kubwa la damu ambalo pia huweza kuchangia uwezekano wa kupata magonjwa mengine sugu kama yale ya figo, moyo na pia mifupa kama "Osteoporosis".

Jinsi ya Kupunguza Matumizi ya Chumvi
1. Mpishi wa familia anahitajika kupunguza chumvi inayowekwa kwenye chakula wakati wa kuandaa au kupika chakula na ni vyema akaambiwa wazi kuhusu madhara yatokanayo na ulaji wa chumvi nyingi.

2. Epuka kuweka chumvi mezani, kwa kuwa huchangia walaji kuongeza chumvi bila hata kuonja.

3. Epuka ulaji wa vyakula vilivyosindikwa kwa kutumia au kuongezwa chumvi, kama nguru aliyekaushwa kwa chumvi pamoja na baadhi ya vyakula vya makopo au paketi.

4. Soma lebo kwa makini wakati wa manunuzi ya bidhaa zako na uchague vyakula vilivyosindikwa bila ya chumvi iliyoongezwa.

5. Jenga utamaduni wa kula vyakula fresh unavyopika mwenyewe kwani itakuwa kwako ni rahisi kutambua kiasi cha chumvi unachotumia.

Kwa mawasiliano zaidi tupigie kwa simu nanmba +255 716 300 200/ +255 784 300 300/ +255 784 300 300.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore ya simu yako kisha tafuta Mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment