Wednesday, 7 June 2017

Hizi hapa aina 7 ya vyakula usivyotakiwa kabisa kuweka kwenye friji


Kwa maisha ya mjini wengi wetu tumekuwa tukitumia friji au jokofu kwa lugha nzuri ya kiswahili kama moja ya chombo cha kuhifadhia vyakula vyetu ili visiharibike.

Familia nyingi zimekuwa na mtindo wa kufanya manunuzi ya mahitaji ya mwezi mzima au wiki nzima ya vyakula na kisha kuhifadhi kwenye jokofu.

Pamoja na uwezo wa friji au jokofu kuweza kufanya vyakula visiharibike haraka, lakini napenda msomaji wangu utambue kuwa si kila tunda,mboga, kiungo au kimiminika kinaweza kuwekwa kwenye friji.

Leo nimekusogezea hii orodha ya vyakula au matunda na mboga ambavyo havipaswi kuwekwa ndani ya friji au jokofu.

1. Nyanya
Kiungo hiki kwanza ni rahisi kuharibika na hivyo kinapowekwa kwenye friji huweza kustahimili kwa muda mrefu bila kuharibika lakini kikubwa utakachokosa kwenye nyanya hiyo ni kutokuwa na ladha.

2. Tikiti Maji
Tunda hili unapoliweka kwenye friji huchangia kupoteza ladha kwa haraka, lakini kwenye suala la kulilinda kuharibika hapo utakuwa umefanikiwa licha ya kupotez ladha yake halisi.

3. Viazi Mviringo.

4. Kitunguu Maji & Swaumu
Ukiweka kiungo hiki kwenye friji utachangia kuanza kuweka ukungu na baadaye kuharika kwa haraka zaidi.

5. Asali
Haakuna haja hata kidogo ya kuweka asali ndani ya friji kutokana na yenyewe kuwa na uwezo wa kujitunza muda mrefu bila kuharibika hata kidogo.

6. Mafuta ya Mzaituni
Kama wewe ni mtumiaji wa mafuta haya kwa kupikia kumbuka kuwa hupaswi kuweka chupa ya mafuta haya ndani ya friji hata kidogo. Badala yake unaweza kuyaweka kabatini tu.

7. Mkate

Asante kwa kuendelea kufuatilia masomo mbalimbali ya afya kupitia mtandao huu najua kwenye somo hili huenda kuna baadhi ya vitu vitakuwa vimekuchanganya labda kwa kuwa hata wewe nyumbani huwa unaweka nyanya, mkate, tikiti maji kwenye friji ukiamini unatunza.

Kama utahitaji ushauri zaidi kuhusu matunda, mbogamboga na lishe bora tupigie kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore ya simu yako kisha tafuta Mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment