Thursday, 15 June 2017

Ifahamu kazi nyingine ya karafuu inapochanganywa na asali


Unapokula chakula mara zote huwa unatarajia kufurahia chakula na si kupata karaha, lakini kuna wakati chakula huweza kuwa kikwazo hasa pale unapokula na kutapika kutokana na kukumbwa na hali ya kichefuchefu.

Kichefuchefu na kutapika mara nyingi huwa na uhusiano na mfumo wa uyeyushaji wa chakula ndani ya tumbo.

Iwapo kutapika kutakuwa kumesababishwa na mzio wa chakula, kula kuzidi kiasi au sumu ndani ya chakula, ni vyema kutapika kuendelee badala ya kuzuia ili chakula chote kilicho tumboni kitoke kwani baada ya kutapika hali itarudi kuwa ya kawaida.

Sasa pale endapo utaona kuna umuhimu au haja ya kuzuia kutapika ili kukinga athari kubwa zinazoweza kujitokeza baadaye ikiwa ni pamoja na mhusika kuishiwa nguvu na maji pia unaweza kutumia njii hii ifutayo:-


Tafuta karafuu kisha saga vipande viwili vya karafuu na uchanganye kijiko kimoja cha mezani cha asali halafu lamba mchanganyiko huo taratibu. Njia hii itasaidia kuacha kutapika mara moja

Kwa maelezo zaidi kuhusu mada hii na nyingine nyingi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment