Friday, 16 June 2017

Je, unaufahamu uwatu? zipo hapa faida zake 5 hasa kwa wanawake

Uwatu au kwa lugha ya kiingereza (fenugreek) ni mmea asili ambao hupatikana Ulaya mashariki na Ethiopia, lakini mmea huu unastawi pia nchini India na Pakistani 

Tanzania mmea huu hulimwa visiwa vya Unguja na Pemba. Mmea huu unastawi hadi kufikia kimo cha sm 30-80.

Leo nataka kuelezea faida za mbegu za uwatu ambazo huweza kusagwa na unga wake kutumika kutoa ahueni kwa matatizo mbalimbali.

Zifuatazo ni faida za unga wa uwatu.

1. Unga wa uwatu ni mzuri kwa kinamama wanaonyonyesha
Hii husaidia kuongeza kiwango cha utokaji na ubora wa maziwa kutokana na uwatu kuwa na kiwango kizuri cha magnesium pamoja na vitamin.

2. Uwatu pia husaidia kupunguza maumivu wakati wa mzunguko kwa wanawake (hedhi).

3. Hupunguza cholesterol mwilini, hali ambayo husaidia kumuepusha mhusika kutozongwa na magonjwa mbalimbali hasa yasiyoambukizwa kama vile mshtuko wa moyo na kiharusi.

4. Hupunguza maumivu ya vidonda vya koo pamoja na kikohozi pia.

5. Husaidia kwa wenye matatizo ya kukosa choo kwani huboresha afya ya mfumo wa umeng'enyaji wa chakula tumboni.

Kwa maelezo zaidi kuhusu mada hii na nyingine nyingi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment