Thursday, 22 June 2017

Kazi 3 za passion mwilini


Passion ni miongoni mwa matunda yenye virutubisho mbalimbali ndani ya mwili ikiwa ni pamoja na vitamin C ambayo husaidia kuimarisha kinga za mwili pamoja vitamin A ambayo husaidia kuboresha afya ya macho.

Zifutazo ni miongoni mwa faida za passion kiafya:-

Hulinda afya ya ngozi
Kutokana na matunda haya kuwa na vitamin C, A za kutosha hivyo passion linakuwa na uwezo mzuri wa kuboresha afya ya ngozi.

Hurekebisha umen'genyaji wa chakula tumboni
Uwezo huu unatokana na kuwa na kiwango cha fiber ndani yake ambacho husaidia kufanya umeng'enyaji wa chakula kuwa mzuri ndani ya tumbo.

Husaidia kuboresha afya ya mifupa
Ndani ya passion kuna madini ya magnesium, copper, phosphorus, ambayo husaidia kuboresha afya ya mifupa ndani ya mwili na kuifanya kuwa imara zaidi.

Kumbuka kuwa unaweza kuwasiliana nasi kwa ushauri zaidi tupigie kwa namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pep dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku


No comments:

Post a Comment