Friday, 2 June 2017

Kazi 6 za mafuta ya kitunguu swaumu, huweza kuondoa chunusi mara moja pia

How to Make Garlic Oil for Natural Remedies: 9 Amazing Ways to Use it
KITUNGUU swaumu ni miongoni mwa viungo vinavyotegemewa katika kuongenza ladha nzuri kwenye vyakula mbalimbali.

Mbali na kiungo hicho kutumika kunogesha vyakula pia kikitumiwa ipasavyo huweza kusaidia kutuliza matatizo kadhaa ya kiafya.

Leo naomba kukueleza kuhusu faida za mafuta ya kiungu hiki (kitunguu swaumu)

1. Husaidia kwa wenye chunusi
Hii ni kutokana na kuwa na na virtubisho hivi vya selenium, allicin, vitamin c copper na zinc ambavyo kwa pamoja huboresha afya ya ngozi

2. Huimarisha kinga za mwili
Matumizi ya mafuta haya pia husaidia kuimarisha kinga za mwili kwani ndani yake kuna vitamin C, B1, B6 pamoja na madini ya chuma na phosphorous.

3, Hutuliza maumivu ya sikio
Kama unasumbuliwa na tatizo la maumivu makali ya sikio unaweza kutumia mafuta haya ya kitunguu swaumu kwa kuweka tone moja la mafuta hayo kwenye sikio lenye tatizo mara moja kwa siku.

4. Hutumika kama njia asili ya kufukuza mbu yanapopakwa mwilini, kwani mbu huchukizwa na harufu yake na kukimbia.

5. Hutuliza maumivu ya meno
Maumivu ya jino yanaweza kutulizwa kwa kutumia mafuta haya ya kitunguu swaumu kwa kuweka kiasi kidogo cha mafuta kwenye eneo lililoathirika.

6. Humaliza tatizo la mba
Unapotumia mafuta haya kwa kuweka kwenye nywele huweza kumaliza shida ya mba na kuzifanya nywele kuwa na afya njema

Kwa maelezo zaidi usisite kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0769 400 800/ 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment