
Je, umekuwa ukihangaishwa na matatizo ya ngozi hasa pale ngozi yako inapokuwa na makunyanzi Sasa badala ya kuhangaika tambua kuwa unaweza kuifanya ngozi yako ianze vizuri kwa kutumia mbinu hizi za asili.
Unachotakiwa kufanya ni kuwa na nyanya, kipande cha papai pamoja na maji safi na salama.
Namna ya kufanya
Pata papi lililoiva menya kisha lisage na kupata ujiuji mzito. Baada ya kutengeneza ujiuji huo, jipake usoni na acha ukauke kwa muda wa dakika 15. Kisha osha na maji ya uvuguvugu na ukausha uso wako kwa taulo safi.
Zoezi hili unaweza kufanya mara mbili kwa siku, kwa muda wa wiki mbili hadi tatu na utaona matokeo yake.
Pia unaweza kutumia nyanya mbivu. ambapo utafanya kama vile ulivyofanya kwa papai.
Zingatia kunywa maji mengi kila siku ili kuweka ngozi yako katika hali ya unyevunyevu zaidi, lakini pia kumbuka kuwa unapotumia mbinu hizi za asili lazima uache kutumia krimu au mafuta yenye kemikali.
Kwa maelezo zaidi kuhusu mada hii na mengine mengi tutafute kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com
No comments:
Post a Comment