Thursday, 8 June 2017

Kifahamu kiungo chenye uwezo wa kutuliza maumivu ya tumbo haraka


Maumivu ya tumbo hukosesha raha na kumfanya mhusika kutokuwa na furaha hata kidogo na wakati mwingine kuharisha.

Mara nyingi tatizo hili huweza kuchangiwa na uyeyushaji mbovu ndani ya tumbo, tumbo kujaa gesi, kiungulia na  ukosefu wa choo.

Hata hivyo, wakati mwingine tatizo hili huweza kuwa ni dalili za matatizo mengine makubwa zaidi kama vile vidonda vya tumbo, ngiri na hata U.T.I pia.

Sasa leo naomba kukwambia msomaji wangu kuhusu tangawizi namna inavyoweza kukusaidia kupunguza maumivu ya tumbo au kumaliza kabisa.

Namna ya Kufanya
Nunua tangawizi zako kadhaa, kisha zikate vipande kadhaa au sisage kiasi kama utaweza halafu ziweke kwenye maji kisha chemsha kama chai.

Baada ya hapo itoe kwenye moto halafu iache iwe ya uvuguvugu kisha weka asali kidogo halafu kunywa mchanganyiko huo taratibu.

Kunywa mchanganyiko huo mara mbili hadi tatu kwa siku na itakusidia kumaliza kabisa maumivu ya tumbo.

Kwa maelezo na ufafanuzi zaidi tupigie kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore ya simu yako kisha tafuta Mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment