Friday, 2 June 2017

Kwa wale wasiojua faida za magome ya mbuyu zipo hapaMagome ya mmbuyu hutokana na mti mkubwa uitwao mbuyu inayopatikana katika ukanda wa tropiki, Matunda yake yanaitwa mabuyu, gamba la tunda hilo huitwa kibuyu na ubuyu ni nyama ya tunda.

Mti huu umesheheni malighafi nyingi na nzuri katika afya ya binadamu, ambapo inaelezwa unga wa ubuyu huwa na vitamin na madini mengi, kwani unga huo una kiasi cha vitamin C nyingi.

Leo nataka kueleza kuhusu magome ya mti huu mkubwa na mnene wa mbuyu yanavyoweza kusaidia kutuliza homa.

Unachopaswa kufanya ni kupata magome ya mbuyu kiasi cha kilo moja halafu yapondeponde na kuyaloweka ndani ya maji safi kiasi cha lita 2 kwa muda wa saa 12 kisha utatumia maji hayo nusu glasi mara tatu kwa siku na yatakusaidia kupunguza makali ya homa au kumaliza kabisa.


Ni vyema kupata maelezo ya kina zaidi kutoka kwetu kabla ya kuanza kutumia magome hayo, wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment