Monday, 5 June 2017

Mafuta ya nazi kwa wenye shida ya kijinyama kwenye njia ya haja kubwaJe, unafahamu kuhusu bawasiri ? Ni ugonjwa unaotokana na kuathirika kwa mishipa ya damu ya ndani na nje ya sehemu ya haja kubwa na wakati mwingine mishipa hiyo huweza kupasuka/kuteleza na kuvuja damu kwenye njia ya haja kubwa na kasababisha kutoka kinyama au uvimbe.

Ugonjwa huu wa bawasiri kwa lugha ya kitaalamu hufahamika kama 'hemorrhoids' tatizo hili huwaathiri watu wote ila zaidi huwaathiri watu wazima kuliko watoto.

Chanzo cha tatizo
Chanzo halisi cha tatizo hili hakijapatikana ila kuna vitu ambavyo huaminika kuwa chanzo cha kupata tatizo hilo la bawasiri ambavyo ni hizi zifuatazo:-

1. Kushiriki mapenzi kinyume na maumbile
2.Kusumbuliwa na tatizo la kukosa choo kwa kipindi kirefu
3. Kupatwa na tatizo la kuharisha kwa kipindi kirefu
4. Umri
5. Kuwa na uzito kupita kiasi
6. Kukaa kwa muda mrefu n.k

Mara nyingi tatizo hili huondolewa kwa kufanyiwa upasuaji mdogo hospitali na kukatwa kinyama hicho. Lakini unaweza kujaribu kutumia njia hii na ikakusaidia endapo tatizo lipo katika hatua za awali.

Tumia mafuta ya nazi

Unachopaswa kufanya ni kuchemsha mafuta ya nazi kisha yaache yapoe na kuwa ya uvuguvugu halafu utatumia kupaka taratibu mafuta hayo sehemu yenye kijinyama hicho au eneo lenye tatizo. fanya hivyo kutwa mara mbili hadi pale utakapoona mabadiliko.

Kwa msaada zaidi wa maelekezo unaweza kuwasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment