Friday, 2 June 2017

Maji yanavyoweza kuwasaidia wenye tatizo la vidonda vya tumbo


Ugonjwa wa vidonda vya tumbo huibuka baada ya kutokea vidonda kwenye kuta za utumbo wa mwanadamu ambavyo  hutokana na kuzidi kwa kiwango cha tindikali yenye kazi ya kuyeyusha chakula kiingiacho mwilini.

Lakini leo naomba kukueleza kuhusu namna maji yanavyoweza kutoa awueni kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo hasa vilivyo katika hatua za awali.

Namna ya Kufanya
Mgonjwa anatakiwa kunywa lita moja ya maji safi na salama alfajiri kabla ya jua kuchomoza na kabla ya kusafisha kinywa au kupata kifungua kinywa.

Kisha mgonjwa anapaswa kusubiri kwa dakika 45 ndipo asafishe kinywa na kupata kifungua kinywa chake cha siku.

Pia wakati wa mchana mgonjwa atapaswa kunywa tena lita 1 ya maji ya kunywa dakika 45 kabla  ya kula chakula cha mchana na usinywe maji yoyote baada ya kula chakula hicho cha mchana kwa dakika 45.

Mbali na hayo, wakati wa usiku pia mgonjwa anapaswa kunywa maji ya lita 1 dakika 45 kabla ya kula chakula cha usiku na akae dakika 45 kabla ya kwenda kulala.

Zingatia
Mbinu hii huchukua muda wa siku 10 mpaka mwezi mmoja kabla ya kupata nafuu. Katika kipindi hiki chote mgonjwa anapaswa kuzingatia masharti juu ya ulaji na vitu vya kuepukwa yaliyoainishwa mwanzoni mwa sura hii.

Kwa maelezo zaidi usisite kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0769 400 800/ 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment