Saturday, 17 June 2017

Mambo 4 ambayo hupaswi kuyafanya mara unapopata ajira yako ya kwanza

Mara nyingi watu huwa tunakuwa na malengo mengi kabla ya kupata ajira au kazi, lakini wengi wetu hujikuta mambo yakienda kinyume na matarajio yetu na kuanza kufanya yale ambayo hatahukupanga.
Leo ninayo mambo kadhaa ambayo hupaswi kuyafanya mara tu unapopata ajira au kazi.

1. Kuchukua Mkopo haraka
Vijana wengi wanapoanza kazi kwa kuwa walikuwa na malengo makubwa bila kujua kiwango cha mshahra hujikuta wakilazimika kukopa mara tu wanapoanza kazi bila kutafakari kwa kina zaidi na baadaye kujikuta wakiumiza kichwa zaidi kwenye kufanya marejesho na hata kukosa pesa ya kujikimu.

2. Kununu vitu vingi kwa mkupuo
Mara unapopata ajira usikimbilie kununua vitu kwa haraka na badala yake nunua taratibu na kwa awamu kwani huwezi jua huenda unachunguzwa kwa muda na baadaye unaweza kuhamishwa kituo cha kazi, hivyo kama utakuwa tayari unavitu vingi inaweza kukuwia ugumu zaidi au kukulazimu kuuza vitu vyako na kuenda kuanza upya tena.

3.Epuka kuanzisha uhusiano wa kimapenzi
Waajiriwa wengi wa mara ya kwanza hujiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi pindi wanapoanza maisha mapya wakiwa kazini na mara nyingi mahusiano hayo huwa hayadumu kutokana na kutokuwa na mapenzi ya dhati zaidi huwa ni mapenzi ya fedha na ndio maana huenda sambamba na kupata kwako ajira. Hivyo watu wanamna hii hujikuta wakipoteza hata ya malengo yao na kuishia kutupa pesa hovyo kwenye mahusiano hayo hasa katika matumizi.

4. Usikurupuke kuanzisha miradi au biashara
Hii pia huweza kuleta picha mbaya kwa muajiri wako, hivyo ni vyema kuwa na subira kabla ya kuanzisha mradi wako wowote au biashara na mara nyingi biashara za kuanzisha kwa namna hiyo hufa kutokana na kutokuwa na malengo endelevu.

Zingatia
Unapoajiriwa kwa mara ya kwanza kumbuka kuwa huo ni muda mzuri wa kusimamia yale malengo yako uliyojipangia awali kabla ya kupata hiyo kazi, lakini pia zingatia kujiwekea akiba kwa huo mshahara unaoupata na kumbuka kupunguza kiwango cha matumizi yasiyo na umuhimu kwa wakati huo.

Pia wengi wanapopata ajira husahau kumkumbuka Mungu wao, lakini tunakumbushana leo kuwa usiache kuendelea kumshukuru Mungu kwa kila hatua yako unayopitia katika maisha yako.

Kwa maelezo au ushauri zaidi kuhusu mada hii na mengine mengi hasa kuhusu lishe bora tutafute kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment