Wednesday, 14 June 2017

Mambo 5 yatakayokuepuhsa kuwa na macho mekundu


Habari za leo mdau wangu wa tovuti hii naamini utakuwa upo vizuri, leo nimeona tufahamishane baadhi ya mambo ambayo yatakusaidia wewe mwenye tatizo la macho yako kuwa mekundu.

Macho kuwa mekundu huweza kusababishwa na sababu mbalimbali zikiwemo za kimazingia pia.

Yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo yakizingatiwa husaidia kuboresha afya ya macho yako.

1. Ulaji wa matunda na mboga za majani
Mbogamboga na matunda huwa na vitamin muhimu kwa ajili ya macho mfano vitamin A,C, na E ambazo kimsingi ndio muhimu sana kwa ajili ya macho. Katika matunda unaweza kutumia tango pia ili kuboresha macho yako zaidi.

2. Kulala kiasi cha kutosha
Wataalam wa masuala ya afya wamekuwa wakipendekeza kuwa binadamu alale angalau saa saba hadi nane kwa siku ili kuurudisha mwili uliochoka katika hali yake ya kawaidi, kwani mtu anayekosa usingizi wa kutosha ni rahisi kwake kuwa na macho mekundu kwa sababu ya uchovu.

3. Unywaji wa maji mengi sana
Kunywa angalau glass 8 mpaka 10 kwa siku ni muhimu sana kwa macho yako kwani maji husafisha mwili wote na kuondoa sumu mwilini. Tambua kuwa kutokunywa maji huweza kuchangia mwili kuwa mkavu na macho kubadilika rangi.

4. Punguza kazi za macho
Hii ni kwa wale ambao hufanya kazi za computer au kuangalia movie hali hiyo nayo huchangia kuchosha macho na hivyo kuweza kuchangia kuwa mekundu.

5. Epuka mazingira yenye vumbi na moshi
Watu ambao huishi katika mazingira hayo huweza kukumbwa na tatizo hilo ndio maana asilimia kubwa ya wakazi wa vijijini hukumbwa na tatizo hili kutokana na matumizi ya kuni ambazo husababisha moshi na baadaye macho kuwa mekundu

Zingatia

Ni vyema kuwaona wataalam wa macho ikiwa unaona tatizo hilo limeendelea kukusumbua kwa muda mrefu, lakini pia jenga utaratibu wa kuchunguza macho yako angalau mara mbili kwa mwaka kama wataalam wa macho wanavyoshauri.

Kwa ushauri zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment