Monday, 12 June 2017

Mambo yamsingi unayotakiwa kuyafanya ukiamka tu!

Mara ngapi unapoamka umejikuta huna amani na huna shahuku ya kufanya chochote? Najua hali hiyo itakuwa imewahi kukuta ukiwa kama binadamu.


Hali hiyo huweza kumkuta mtu yoyote katika maisha ya kila siku, lakini hapa ninayo mambo muhimu ya kuyazingatia ili asubuhi yako iende vizuri na uweze kuendelea na shughuli zako za kila siku.

1. Amka mapema
Unapoamka mapema husaidia siku yako kwenda vizuri kwa kuwa utapata muda wa kutosha wa kupangilia mambo yako. Hivyo ni vyema ukalala mapema na kuamka mapema ili mwili wako uweze kupata mapumziko mazuri kwa ajili ya kazi za siku inayofuata.

2. Sala/ Maombi
Kusali ni muhimu kwako na wakati huo huo pia utakuwa ukiipatia akili yako hali ya ukimya. Unaposali kutokana na imani yako kwa kiasi kikubwa husaidia kufungua milango yako ya baraka katika shughuli zako za siku husika.

3. Soma Kitabu
Licha ya kwamba si utamaduni wa wengi wetu wa kusoma hasa asubuhi, lakini ni wakati mzuri zaidi wa kuingiza mambo mazuri kichwani kabla ya kelele za dunia hazijaanza. Hakikisha vitabu unavyosoma ni vile vyenye kukupatia maarifa.

4. Andaa ratiba ya siku yako
Epuka kuanza siku yako bila ratiba kwani ni sawa na kuanza safari ya kuelekea usikokujua. Orodhesha mambo utakayofanya katika siku hiyo.

Kwa ushauri zaidi hasa kuhusu lishe bora unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore ya simu yako kisha tafuta Mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment