Thursday, 8 June 2017

Mandai amekuletea mchanganyiko wenye uwezo wa kukukinga dhidi ya magonjwa


Mtindo wa maisha ni miongoni mwa sababu ambazo huweza kuchangia afya njema kwa binadam au kuwa na afya mbovu.

Unaposikia neno mtindo wa maisha hujumuisha kuhusu namna unavyokula, kunywa na shughuli zote unazofanya kila siku.

Kuna aina kadhaa ya magonjwa ambayo hutokana na utamaduni wa namna watu wanavyokula ambapo baadhi hujikuta wakiingia kwenye matatizo kadhaa ya kiafya.

Matatizo hayo ni pamoja na kisukari, shinikizo la damu, matatizo ya moyo, vidonda vya tumbo n.k.

Sasa basi kutokana na kulitambua hilo sisi Mandai Product ambao tunashughulika na uandaaji wa virutubisho na lishe tumeona ni vyema kuwaletea huduma za lishe bora asilia.

Akizungumza na mtandao huu Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Abdallah Mandai (pichani hapo juu) anasema kuwa njia mojawapo ya kuepuka magonjwa mbalimbali hasa yasiyoyakuambukizwa ni kutokula vyakula ambavyo havitaleta shida baadaye.

Kutokana na kutambua hilo Mtaalam Mandai anasema kuwa, kwa sasa wameandaa lishe kwa makundi mbalimbali, wakiwemo wazee, watoto na watu wa kawaida.

Lishe hiyo iliyopo kwenye mfumo wa kimiminika (juisi) inamchanganyiko wa matunda ya stafeli, mbegu za papai, tui la nazi, unga wa ubuyu pamoja na uyoga ambapo kila kimoja katika mchanganyiko huo kina faida zake ndani ya mwili  kama ambavyo Mtaalam Mandai anafafanua hapa chini:-

1. Tunda la Stafeli
Tunda hili lina kiwango kizuri cha vitamin C, madini ya calcium na chuma ambayo yote hutoa msaada ndani ya mwili na kumfanya mhusika kuwa na nguvu na kinga imara.

2. Unga wa Ubuyu
Ndani ya unga wa ubuyu kunakiwango kikubwa cha vitamin C pia pamoja na wanga kwa asilimia 4.2, bila kusahau nyuzinyuzi sambamba na madini ya chokaa na vitamin A.

3. Unga wa Papai
Unga huu husaidia kukinga dhidi ugonjwa wa malaria, ambapo ili kuupata unachukua mbegu za papai na kuzisaga na kutengeneza juisi.

Pia unga huu husaidia kupunguza tindikali ndani ya tumbo na hivyo kuwa msaada kwa wenye tatizo la vidonda vya tumbo.

4. Tui la Nazi
Mtaalam Mandai anasema kuwa tui hilo husaidia kuondoa mafuta kwenye mishipa ya damu, huepusha homa ya tumbo na kuimarisha afya ya mmeng'enyo wa chakula  na hivyo kumuepusha mhusika dhidi ya tatizo la kutopata choo.

5. Uyoga
Mmea huu unaeleza kuwa huongeza kwa kiasi kikubwa kinga za mwili kwani ndani yake unapata protini asilimia 20 hadi 45 unapata madini ya chuma na calcium ambayo husaidia kuondoa hali ya uchovu.

Muda wa kunywa mchanganyiko huo  
Mtaalama Mandai anasema mchanganyiko huu wa juisi unatakiwa kutumiwa siku saba hadi mwezi mmoja, ambapo utaona mabadiliko ndani ya mwili wako.

Kwa ujumla juisi hii huongeza nguvu kwa kinababa na kuepusha uvimbe kwa kinamama (fibroid )  pamoja na kuondoa uchovu na kuimarisha afya ya akili

Kwa ufafanuzi zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore ya simu yako kisha tafuta Mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment