Thursday, 22 June 2017

Matatizo 8 ya kiafya ambayo yanasababisha mwanamke kuumwa kiuno

Matatizo ya maumivu ya kiuno ni tatizo linalosumbua wanawake wengi mara kwa mara na hasa hujitokeza wakati wa hedhi.

Hata hivyo, kuna baadhi ya maumivu ya kiuno ambayo hukaa kwa muda mrefu mpaka miezi sita na kuendelea au kujirudia mara kwa mara kwa muda mrefu.

Zifuatazo ni baadhi ya sababu 8 ambazo huweza kuchangia maumivu hayo ya muda mrefu ya kiuno.
1.Maambukizi ya njia ya mkojo ya muda mrefu

2. Maambukizi ya via vya uzazi

3. Maambukizi ya kibofu cha mkojo

4. Ikiwa mhusika aliwahi kupata ajali iliyomuathiri maeneo ya kiuno

5. Kusagika kwa mifupa kwenye maungo

6. Maumbukizi ya ndani ya kiuno ya muda mrefu

7. Mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi

8. Uvimbe kwneye mirija ya uzazi

Zingatia

Unapopatwa na maumivu ya kiuno ya muda mrefu kumbuka kuwa matibabu yake huzingatia kwa kugundua kwanza chanzo cha maumivu hayo, yaani kujua historia ya tatizo pamoja na mhusika kufanyiwa uchunguzi pamoja na vipimo. Hivyo matibabu yake hutegemea na chanzo cha tatizo.

Kama utahitaji ushauri pia kutoka kwetu unaweza kuwasiliana na Mtaalam wa lishe Abdallah Mohammed Mandai kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku


No comments:

Post a Comment