Tuesday, 27 June 2017

Mchanganyiko wa matunda ya aina 3 wenye kuimarisha kinga za mwili

Mara kadhaa tumekuwa tukisikia usemi wa waswahili wakisema kuwa kinga ni bora kuliko tiba, hivyo na mimi leo nimeona nikueleze msomaji wangu kuhusu huu mchanganyiko wenye uwezo wa kusaidia kuimarisha zaidi kinga zako za mwili.

Mchanganyiko huu ni wa matunda mbalimbali ambayo sote tunayafahamu na huenda tumekuwa tukiyatumia mara kwa mara.

Sasa matunda hayo ni tikitimaji, apple, pamoja na juisi ya karoti vinapaswa kuchanganywa pamoja na kupata mchanganyiko mmoja kisha mhusika kunywa glasi moja asubuhi na jioni na hii husaidia kuimarisha kinga za mwili.

Unachotakiwa kufanya ni kukata vipande vya tikitikimaji na kuondoa mbegu zake kisha hivyo hivyo kwenye apple na uondoe pia mbegu halafu saga kwa pamoja na upande mchanganyiko wake

Baada ya hapo chukua karoti zako na uzioshe kisha saga ili kupata juisi yake halafu utaichanganya pamoja na ule mchanganyiko wa awali wa tikiti pamoja na apple.

Unaweza kuongea nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 kama utakuwa na swali lolote au unahitaji ushauri wa kiafya hasa kuhusu lishe bora.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment