Tuesday, 6 June 2017

Mengine zaidi yakuyajua kuhusu faida za soyaSoya ni jamii ya mikunde na inasifika kwa kuwa chanzo kizuri cha protini katika lishe ya binadamu. 

Soya ina protini nyingi, hivyo huweza kutumika kama mbadala wa matumizi ya nyama.

Virutubisho vilivyomo ndani yake
Soya ina virutubisho vingi ikiwa ni pamoja na protini, madini ya calcium, vitamini B, Omega -6 na kambakamba (fiber). Pamoja na hayo, soya pia husaidia kupunguza Lehemu Mwilini.

Pia kuna baadhi ya tafiti zilizowahi kuainisha kuwa wanawake wanaotumia soya kwa wingi katika mlo wao huwa na hatari ndogo ya kupata saratani ya matiti. Hii inadhaniwa ni kutokana na kampaundi za isoflavones. Hata hivyo bado hakujakuwa na ushahidi wa kutosha kitafiti kuthibitisha hilo.

Kuhusu Matumizi yake zaidi
Soya hutumika kutengeneza vyakula vya aina nyingi. Unaweza ukatumia soya kama maziwa, kama chai, lakini kumbuka kuwa lazima soya ipikwe vizuri katika matumizi yake

Kwa ufafanuzi zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com


Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore ya simu yako kisha tafuta Mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment