Friday, 2 June 2017

Mtaalam Mandai kakuletea faida za matunda haya ya aina 5


Zipo faida nyingi za kula matunda na kama ambavyo tunafahamu matunda yana virutubisho vingi ikiwa ni pamoja na vitamin A na C ambazo hupatikana kwenye matunda mengi ukilinganisha na virutubisho vingine vilivyopo kwenye matunda mengine.

Kwa ujumla matunda yanafaida mbalimbali ndani ya miili yetu ikiwa ni pamoja na kupunguza uwezekano wa matatizo ya moyo, kiharusi pamoja na mrundikano wa sumu mwilini yaani cholesterol.

Kimsingi kila aina ya tunda huwa na faida zake mwilin, lakini leo napenda ufahamu kuhusu hizi faida za matunda haya yafuatayo;-

1. PARACHICHI
a) Ni chanzo kizuri cha vitamin E.
b) Hupunguza kiwango cha cholesterol mwilini.
c) Huboresha afya ya ngozi

2. NDIZI
a) Ni chanzo cha nishati mwilini
b) Chanzo cha vitamin B6 na madini ya potassium.
c)Hupunguza uwezekano wa shinikizo la damu
d) Hulinda afya ya mifupa.


3. ZABIBU
a)Hukuweka mbali na maradhi ya moyo
b)Husaidia kuongeza damu mwilini
c) Ni chanzo cha madini ya manganese.

4. EMBE.
a) Ni chanzo cha vitamin A na E.
b)Ni tunda nzuri kwa afya ya ngozi
c) Huimarisha afya ya nywele
d) Huimarisha uwezo wa kuona vizuri.


5. CHUNGWA.
a)Ni chanzo cha vitamin C
b)Huimarisha kinga za mwili
c)Hupunguza uwezekano wa ukosefu wa choo
d)Huzuia matatizo ya homa sambamba na mafua.

Kwa maelezo zaidi au ufafanuzi kuhusu matumizi ya lishe na ulaji bora unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment